An eulogy of Mzee (Elder) Kirimi M'Marete M'Muthamia Mpuria, the author's father, upon his demise on July 5, 2005.
Na Mwiti-o-M'Marete, Malenga wa Mlima Meru
Mwisho wa mti ni tunda,uzaapo likalika
Hesabu ni hadi kenda,ndiposa hukamilika
Nayo maisha ni kwenda, Akhera kwenye baraka
Buriani wetu Baba,wendako wende kwa kheri.
Yako imekamilika,kazi isiyo kifani
Jinsi ’livyokuchosha,unabarizi mbinguni
Mpendwa tumekupisha,Mola akupe amani
Buriani wetu Baba,wendako wende kwa kheri.
Twajua ulipo Baba,katua ukatuama
Huna kilichokukaba,walala u wakoroma
Tena huna ’lichobeba,mizigo kaacha nyuma
Buriani wetu Baba, wendako wende kwa kheri.
Baba ulituusia,mja ni haki na kazi
Nasi twakuahidia,kamwe hatutoajizi
Nyayo zako ’tafwatia,wasia wako azizi
Buriani wetu Baba, wendako wende kwa kheri.
Baba pole kwa safari,’mefika katangulia
Tutetee kwa Kahari,pema akatutengea
Ndipo yetu ’tapojiri,ndiwe tatuonya njia
Buriani wetu Baba, wendako wende kwa kheri.
Ila adui twahofu,yule mui mwenye inda
Pamwe na njaa sumbufu,na ndwezi zenye kukinda
Nani atayetukifu,haupo ukatulinda?
Buriani wetu Baba, wendako wende kwa kheri.
Jinalo halitozama,talilinda kwa vizazi
’Takuwa mfano mwema,’tazidisha yako kazi
Hadi Siku ya Kiama,tutapokutana tena
Buriani wetu Baba, wendako wende kwa kheri.
*Shairi hili lilitungwa na familia ya Marehemu Mzee M’Marete M’Muthamia aliyetupa mkono wa heri tarehe 5 Julai 2005, na kukaririwa kwenye sherehe ya kumsindikiza mnamo tarehe 15 Julai 2005, Marurui, Meru. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahali pema peponi.
BLIND!
Ross Miller doesn’t have anything to live for anymore. An RPG attack in Afghanistan left him blind and he thought helpless.
He tried going home but that didn’t work out. Luke and Amber Owens who were both wounded in the same